Dan. 5:23-28 Swahili Union Version (SUV)

23. Bali umejiinua juu ya Bwana wa mbingu; nao wamevileta vyombo vya nyumba yake mbele yako; na wewe, na wakuu wako, na wake zako, na masuria wako, mmevinywea; nawe umeisifu miungu ya fedha na ya dhahabu na ya shaba, na ya chuma, na ya mti, na ya mawe; wasioona, wala kusikia, wala kujua neno lo lote; na Mungu yule, ambaye pumzi yako i mkononi mwake, na njia zako zote ni zake, hukumtukuza.

24. Ndipo kile kitanga cha ule mkono kikaletwa kutoka mbele zake, na maandiko haya yameandikwa.

25. Na maandiko yaliyoandikwa ni haya; MENE, MENE, TEKELI, NA PERESI.

26. Na tafsiri ya maneno haya ni hii; MENE, Mungu ameuhesabu ufalme wako na kuukomesha.

27. TEKELI, umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka.

28. PERESI, ufalme wako umegawanyika, nao wamepewa Wamedi na Waajemi.

Dan. 5