6. Aitikisaye dunia itoke mahali pake,Na nguzo zake hutetema.
7. Aliamuruye jua, nalo halichomozi;Nazo nyota huzipiga muhuri.
8. Ambaye peke yake ni mwenye kuzitandika mbingu,Na kuyakanyaga mawimbi ya bahari.
9. Yeye afanyaye hizo nyota za Dubu, na Orioni, na hicho Kilimia,Na makundi ya nyota ya kusini.
10. Atendaye mambo makuu yasiyotafutikana;Naam, mambo ya ajabu yasiyohesabika.
11. Tazama, yuaenenda karibu nami, nisimwone;Tena yuapita kwenda mbele, nisimtambue.
12. Tazama, yuakamata, ni nani awezaye kumzuia?Ni nani awezaye kumwuliza, Wafanya nini?
13. Mungu haondoi hasira zake;Hao wamsaidiao Rahabu huinama chini yake.
14. Je! Mimi nitamjibuje,Na kuyachagua maneno yangu kuhojiana naye?
15. Ambaye, nijapokuwa mimi ni mwenye haki, nisingemjibu;Ningemsihi-sihi mtesi wangu.
16. Kama ningemwita, naye akaniitikia;Hata hivyo singeamini kuwa amesikiza sauti yangu.
17. Yeye anipondaye kwa dhoruba,Na kuziongeza jeraha zangu pasipokuwa na sababu.
18. Haniachi nipate kuvuta pumzi,Lakini hunijaza uchungu.