Ayu. 9:22-24 Swahili Union Version (SUV)

22. Hayo yote ni mamoja; kwa hiyo nasema,Yeye huangamiza wakamilifu na waovu pia.

23. Kama hilo pigo likiua ghafula,Atayadhihaki majaribu yake asiye na kosa.

24. Dunia imetiwa mkononi mwa waovu;Yeye hufunika nyuso za waamuzi wake;Kama si yeye, ni nani basi?

Ayu. 9