18. Haniachi nipate kuvuta pumzi,Lakini hunijaza uchungu.
19. Kama tukitaja nguvu za mashujaa, tazama yupo hapo!Kama tukitaja hukumu, ni nani atakayeniwekea muhula?
20. Ingawa ni mwenye haki, kinywa changu mwenyewe kitanihukumu;Ingawa ni mkamilifu, kitanishuhudia kuwa ni mpotovu.
21. Mimi ni mkamilifu; siangalii nafsi yangu;Naudharau uhai wangu.
22. Hayo yote ni mamoja; kwa hiyo nasema,Yeye huangamiza wakamilifu na waovu pia.
23. Kama hilo pigo likiua ghafula,Atayadhihaki majaribu yake asiye na kosa.
24. Dunia imetiwa mkononi mwa waovu;Yeye hufunika nyuso za waamuzi wake;Kama si yeye, ni nani basi?
25. Basi siku zangu zina mbio kuliko tarishi;Zakimbia, wala hazioni mema.
26. Zimepita kama merikebu ziendazo mbio;Mfano wa tai ayashukiaye mawindo.