11. Tazama, yuaenenda karibu nami, nisimwone;Tena yuapita kwenda mbele, nisimtambue.
12. Tazama, yuakamata, ni nani awezaye kumzuia?Ni nani awezaye kumwuliza, Wafanya nini?
13. Mungu haondoi hasira zake;Hao wamsaidiao Rahabu huinama chini yake.
14. Je! Mimi nitamjibuje,Na kuyachagua maneno yangu kuhojiana naye?
15. Ambaye, nijapokuwa mimi ni mwenye haki, nisingemjibu;Ningemsihi-sihi mtesi wangu.
16. Kama ningemwita, naye akaniitikia;Hata hivyo singeamini kuwa amesikiza sauti yangu.
17. Yeye anipondaye kwa dhoruba,Na kuziongeza jeraha zangu pasipokuwa na sababu.
18. Haniachi nipate kuvuta pumzi,Lakini hunijaza uchungu.
19. Kama tukitaja nguvu za mashujaa, tazama yupo hapo!Kama tukitaja hukumu, ni nani atakayeniwekea muhula?
20. Ingawa ni mwenye haki, kinywa changu mwenyewe kitanihukumu;Ingawa ni mkamilifu, kitanishuhudia kuwa ni mpotovu.