1. Ndipo Ayubu akajibu, na kusema,
2. Kweli najua kuwa ndivyo hivyo;Lakini mtu huwaje mwenye haki mbele za Mungu?
3. Kama akipenda kushindana naye,Hawezi kumjibu neno moja katika elfu.
4. Yeye ni mwenye hekima moyoni, na mwenye uwezo katika nguvu;Ni nani aliyejifanya kuwa mgumu juu yake, naye akafanikiwa?
5. Aiondoaye milima, nayo haina habari,Akiipindua katika hasira zake.
6. Aitikisaye dunia itoke mahali pake,Na nguzo zake hutetema.
7. Aliamuruye jua, nalo halichomozi;Nazo nyota huzipiga muhuri.
8. Ambaye peke yake ni mwenye kuzitandika mbingu,Na kuyakanyaga mawimbi ya bahari.