6. Siku zangu hupita upesi kuliko chombo cha kufumia,Nazo zapita pasipokuwa na matumaini.
7. Kumbuka ya kwamba maisha yangu ni upepo;Jicho langu halitaona mema tena.
8. Jicho lake huyo anionaye halitaniangalia tena;Macho yako yatanielekea, lakini sitakuwapo.
9. Kama vile wingu likomavyo na kutoweka,Ni vivyo huyo ashukaye kuzimuni hatazuka tena kabisa.
10. Hatarudi tena nyumbani kwake,Wala mahali pake hapatamjua tena.
11. Kwa hiyo sitakizuia kinywa changu;Nitanena kwa mateso ya roho yangu;Nitalia kwa uchungu wa nafsi yangu.
12. Je! Mimi ni bahari, au je! Ni nyangumi?Hata ukawaweka walinzi juu yangu?
13. Hapo nisemapo, kitanda changu kitanituza moyo,Malazi yangu yatanipunguzia kuugua kwangu;
14. Ndipo unitishapo kwa ndoto,Na kunitia hofu kwa maono;
15. Hata nafsi yangu huchagua kunyongwa,Na kuchagua kifo kuliko maumivu yangu haya.
16. Ninadhoofika; sitaishi sikuzote;Usinisumbue, kwani siku zangu ni uvuvio.