Ayu. 7:13-16 Swahili Union Version (SUV)

13. Hapo nisemapo, kitanda changu kitanituza moyo,Malazi yangu yatanipunguzia kuugua kwangu;

14. Ndipo unitishapo kwa ndoto,Na kunitia hofu kwa maono;

15. Hata nafsi yangu huchagua kunyongwa,Na kuchagua kifo kuliko maumivu yangu haya.

16. Ninadhoofika; sitaishi sikuzote;Usinisumbue, kwani siku zangu ni uvuvio.

Ayu. 7