Ayu. 7:1-8 Swahili Union Version (SUV)

1. Je! Mtu hana wakati wake wa vita juu ya nchi?Na siku zake, je! Si kama siku za mwajiriwa?

2. Kama mtumishi atamaniye sana kile kivuli,Kama mwajiriwa anayetazamia mshahara wake;

3. Ni vivyo nami nimepewa miezi ya ubatili iwe fungu langu,Nami nimeandikiwa masiku yenye kuchokesha.

4. Hapo nilalapo chini, nasema,Nitaondoka lini? Lakini usiku huwa mrefu;Nami nimejawa na kujitupa huku na huku hata kupambazuke.

5. Mwili wangu unavikwa mabuu na madongoa ya udongo;Ngozi yangu hufumba, kisha ikatumbuka tena.

6. Siku zangu hupita upesi kuliko chombo cha kufumia,Nazo zapita pasipokuwa na matumaini.

7. Kumbuka ya kwamba maisha yangu ni upepo;Jicho langu halitaona mema tena.

8. Jicho lake huyo anionaye halitaniangalia tena;Macho yako yatanielekea, lakini sitakuwapo.

Ayu. 7