7. Roho yangu inakataa hata kuvigusa;Kwangu mimi ni kama chakula kichukizacho.
8. Laiti ningepewa haja yangu,Naye Mungu angenipa neno hilo ninalolitamani sana!
9. Kwamba Mungu angekuwa radhi kuniseta;Kwamba angeulegeza mkono wake na kunikatilia mbali!
10. Hapo ndipo ningefarijika hata sasa;Naam, ningejikuza katika maumivu yasiyoniacha;Kwa kuwa sikuyakana maneno yake Mtakatifu.
11. Nguvu zangu ni zipi, hata ningoje?Na mwisho wangu ni nini, hata nisubiri?
12. Je! Nguvu zangu ni nguvu za mawe?Au mwili wangu, je! Ni shaba?
13. Je! Si kwamba sina msaada ndani yangu.Tena kwamba kufanikiwa kumeondolewa mbali nami?
14. Kwake huyo atakaye kuzima roho inapasa atendewe mema na rafiki;Hata kwake huyo aachaye kumcha Mwenyezi.
15. Ndugu zangu wametenda udanganyifu kama kijito cha maji.Mfano wa fumbi la vijito vipitavyo.
16. Vilivyokuwa vyeusi kwa sababu ya barafu,Ambamo theluji hujificha.
17. Wakati vipatapo moto hutoweka;Kukiwako hari, hukoma mahali pao.