Ayu. 6:20-30 Swahili Union Version (SUV)

20. Wametahayari kwa sababu walitumaini;Wakaja huku, nao walifadhaika.

21. Kwani sasa ninyi mmekuwa vivyo;Mwaona jambo la kutisha, mkaogopa.

22. Je! Nilisema, Nipeni?Au, Nitoleeni toleo katika mali yenu?

23. Au, Niokoeni na mkono wa adui?Au, Nikomboeni na mikono ya hao waoneao?

24. Nifunzeni, nami nitanyamaa kimya;Mkanijulishe ni jambo gani nililokosa.

25. Jinsi yafaavyo maneno ya uelekevu!Lakini kuhoji kwenu, je! Kumeonya nini?

26. Je! Mwafikiri kuyakemea maneno?Maana maneno ya huyo aliyekata tamaa ni kama upepo.

27. Naam, mwapenda kuwapigia kura hao mayatima,Na kufanya biashara ya rafiki yenu.

28. Sasa basi iweni radhi kuniangalia;Kwani hakika sitanena uongo usoni penu.

29. Rudini, nawasihi, lisiwe neno la udhalimu;Naam, rudini tena, neno langu ni la haki.

30. Je! Mna udhalimu ulimini mwangu?Je! Makaakaa yangu hayatambui mambo ya madhara?

Ayu. 6