16. Vilivyokuwa vyeusi kwa sababu ya barafu,Ambamo theluji hujificha.
17. Wakati vipatapo moto hutoweka;Kukiwako hari, hukoma mahali pao.
18. Misafara isafiriyo kwa njia yao hugeuka;Hukwea kwenda barani, na kupotea.
19. Misafara ya Tema huvitazama,Majeshi ya Sheba huvingojea.
20. Wametahayari kwa sababu walitumaini;Wakaja huku, nao walifadhaika.
21. Kwani sasa ninyi mmekuwa vivyo;Mwaona jambo la kutisha, mkaogopa.
22. Je! Nilisema, Nipeni?Au, Nitoleeni toleo katika mali yenu?
23. Au, Niokoeni na mkono wa adui?Au, Nikomboeni na mikono ya hao waoneao?
24. Nifunzeni, nami nitanyamaa kimya;Mkanijulishe ni jambo gani nililokosa.
25. Jinsi yafaavyo maneno ya uelekevu!Lakini kuhoji kwenu, je! Kumeonya nini?
26. Je! Mwafikiri kuyakemea maneno?Maana maneno ya huyo aliyekata tamaa ni kama upepo.
27. Naam, mwapenda kuwapigia kura hao mayatima,Na kufanya biashara ya rafiki yenu.
28. Sasa basi iweni radhi kuniangalia;Kwani hakika sitanena uongo usoni penu.
29. Rudini, nawasihi, lisiwe neno la udhalimu;Naam, rudini tena, neno langu ni la haki.