1. Ndipo Ayubu akajibu na kusema,
2. Laiti uchungu wangu ungepimwa,Na msiba wangu kutiwa katika mizani pamoja!
3. Kwa kuwa sasa ungekuwa mzito kuliko mchanga wa bahari;Kwa hiyo maneno yangu yamekuwa ya haraka.
4. Kwa kuwa mishale ya huyo Mwenyezi i ndani yangu,Na roho yangu inainywa sumu yake;Vitisho vya Mungu vimejipanga juu yangu.
5. Je! Huyo punda-mwitu hulia akiwa na majani?Au, ng’ombe hulia malishoni?
6. Je! Kitu kisicho na ladha yumkini kulika pasipo chumvi?Au je, uto wa yai una tamu iwayo yote?
7. Roho yangu inakataa hata kuvigusa;Kwangu mimi ni kama chakula kichukizacho.
8. Laiti ningepewa haja yangu,Naye Mungu angenipa neno hilo ninalolitamani sana!