1. Ndipo Ayubu akajibu na kusema,
2. Laiti uchungu wangu ungepimwa,Na msiba wangu kutiwa katika mizani pamoja!
3. Kwa kuwa sasa ungekuwa mzito kuliko mchanga wa bahari;Kwa hiyo maneno yangu yamekuwa ya haraka.
4. Kwa kuwa mishale ya huyo Mwenyezi i ndani yangu,Na roho yangu inainywa sumu yake;Vitisho vya Mungu vimejipanga juu yangu.
5. Je! Huyo punda-mwitu hulia akiwa na majani?Au, ng’ombe hulia malishoni?
6. Je! Kitu kisicho na ladha yumkini kulika pasipo chumvi?Au je, uto wa yai una tamu iwayo yote?