9. Yeye afanyaye mambo makuu, yasiyotambulikana;Mambo ya ajabu yasiyo na hesabu;
10. Yeye atoaye mvua inyeshe juu ya nchi,Na kuyapeleka maji mashambani;
11. Awainuaye juu hao walio chini;Na hao waombolezao hukuzwa wawe salama.
12. Yeye huyatangua mashauri ya wadanganyifu,Mikono yao isipate kuyatimiza makusudi yao.
13. Yeye huwanasa wenye hekima katika hila yao wenyewe;Na mashauri ya washupavu yaharibika kwa haraka.
14. Wao hupatwa na giza wakati wa mchana,Hupapasa mchana vilevile kama usiku.