Ayu. 5:20-27 Swahili Union Version (SUV)

20. Wakati wa njaa atakukomboa na mauti;Na vitani atakukomboa na nguvu za upanga.

21. Utafichwa na mapigo ya ulimi;Wala usiogope maangamizo yatakapokuja.

22. Wewe utayacheka maangamizo na njaa;Wala hutawaogopa wanyama wakali wa nchi.

23. Kwani utakuwa na mapatano na mawe ya bara;Nao wanyama wa bara watakuwa na amani kwako.

24. Nawe utajua ya kwamba hema yako ina salama;Na zizi lako utaliaua, wala usikose kitu.

25. Tena utajua ya kwamba uzao wako utakuwa mwingi,Na vizazi vyako watakuwa kama nyasi za nchi.

26. Utafika kaburini mwenye umri mtimilifu,Kama mganda wa ngano ulivyo wakati wake.

27. Tazama, haya tumeyapeleleza, ndivyo yalivyo;Yasikie, uyajue, ili upate mema.

Ayu. 5