Ayu. 5:1-9 Swahili Union Version (SUV)

1. Haya, ita sasa; je! Yuko atakayekujibu?Nawe utamwelekea yupi katika hao watakatifu?

2. Kwani hasira humwua mtu mpumbavu,Nao wivu humwua mjinga.

3. Nimewaona wapumbavu wakishusha mizizi;Lakini mara niliyalaani maskani yake.

4. Watoto wake wako mbali na wokovu,Nao wamesongwa langoni,Wala hapana atakayewaponya.

5. Mavuno yake wale wenye njaa huyala,Na kuyatwaa hata kuyatoa miibani,Nao wenye kiu huzitwetea mali zao.

6. Kwani taabu haitoki mchangani,Wala mashaka hayachipuki katika nchi;

7. Lakini mwanadamu huzaliwa ili apate mashaka,Kama cheche za moto zirukavyo juu.

8. Lakini mimi ningemtafuta Mungu,Ningemwekea Mungu daawa yangu;

9. Yeye afanyaye mambo makuu, yasiyotambulikana;Mambo ya ajabu yasiyo na hesabu;

Ayu. 5