Ayu. 42:1-7 Swahili Union Version (SUV)

1. Ndipo Ayubu akamjibu BWANA, na kusema.

2. Najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote,Na ya kuwa makusudi yako hayawezi kuzuilika.

3. Ni nani huyu afichaye mashauri bila maarifa?Kwa maana, nimesema maneno nisiyoyafahamu,Mambo ya ajabu ya kunishinda mimi, nisiyoyajua.

4. Sikiliza, nakusihi, nami nitanena;Nitakuuliza neno, nawe niambie.

5. Nilikuwa nimesikia habari zako, kwa kusikia kwa masikio;Bali sasa jicho langu linakuona.

6. Kwa sababu hiyo najichukia nafsi yangu, na kutubuKatika mavumbi na majivu.

7. Basi ikawa, baada ya BWANA kumwambia Ayubu maneno hayo, BWANA akamwambia huyo Elifazi Mtemani, Hasira zangu zinawaka juu yako, na juu ya hao rafiki zako wawili; kwa kuwa ninyi hamkunena yaliyo sawa katika habari zangu, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu.

Ayu. 42