8. Mwekee mkono wako;Vikumbuke vile vita, wala usifanye tena.
9. Tazama, kumtamani ni bure;Je! Hatambwaga chini huyo atakayemtazama?
10. Hapana aliye mkali hata akathubutu kumwamsha;Bali ni nani awezaye kusimama mbele yangu mimi?
11. Ni nani aliyetangulia kunipa hata nimlipe?Kila kilicho chini ya mbingu nzima ni changu.
12. Sitanyamaa kusema habari za via vyake,Wala nguvu zake kuu, wala umbo lake zuri.
13. Ni nani awezaye kumbambua magamba yake?Ni nani atakayepenya dirii yake maradufu?
14. Ni nani awezaye kuifungua milango ya uso wake?Meno yake yatisha kandokando yake.
15. Magamba yake yenye nguvu ndiyo fahari yake,Yamefungamana pamoja kama kwa kufungwa kwa muhuri.
16. Jinsi yalivyoshikamanaHata upepo hauwezi kupita kati.
17. Yamefungamana pamoja;Yameshikamana, hata hayawezekani kutengwa.
18. Kwa kuchemua kwake mwanga humemetuka,Na macho yake yanafanana na makope ya alfajiri.
19. Mienge iwakayo hutoka kinywani mwake,Na macheche ya moto huruka nje.
20. Moshi hutoka katika mianzi ya pua yake,Kama nyungu ikitokota, na manyasi yawakayo.
21. Pumzi zake huwasha makaa,Na miali ya moto hutoka kinywani mwake.
22. Katika shingo yake hukaa nguvu,Na utisho hucheza mbele yake.
23. Manofu ya nyama yake hushikamana;Yanakazana juu yake; hayawezi kuondolewa.