3. Je! Atakusihi sana?Au, atakuambia maneno ya upole?
4. Je! Atafanya agano pamoja nawe,Umtwae kuwa mtumishi wako milele?
5. Je! Utamchezea kama ndege?Au, kumfunga kwa ajili ya wasichana wako?
6. Je! Vikosi vya wavuvi watamfanyia biashara?Watamgawanya kati ya wafanyao biashara?
7. Je! Waweza kuijaza ngozi yake na vyuma vyenye ncha,Au kichwa chake kwa vyusa?
8. Mwekee mkono wako;Vikumbuke vile vita, wala usifanye tena.
9. Tazama, kumtamani ni bure;Je! Hatambwaga chini huyo atakayemtazama?
10. Hapana aliye mkali hata akathubutu kumwamsha;Bali ni nani awezaye kusimama mbele yangu mimi?
11. Ni nani aliyetangulia kunipa hata nimlipe?Kila kilicho chini ya mbingu nzima ni changu.
12. Sitanyamaa kusema habari za via vyake,Wala nguvu zake kuu, wala umbo lake zuri.
13. Ni nani awezaye kumbambua magamba yake?Ni nani atakayepenya dirii yake maradufu?
14. Ni nani awezaye kuifungua milango ya uso wake?Meno yake yatisha kandokando yake.