27. Yeye huona chuma kuwa kama nyasi,Na shaba kama mti uliooza.
28. Mshale hauwezi kumkimbiza;Na mawe ya teo kwake hugeuka kuwa kama makapi.
29. Marungu huhesabiwa kama mabua;Naye hucheka mshindo wa mkuki ukitupwa.
30. Pande zake za chini ni kama vigae vikali;Hutandika malazi kama kuweka chombo cha kupuria nafaka juu ya matope.
31. Yeye huchemsha kilindi mfano wa nyungu;Hufanya bahari kuwa kama mafuta.
32. Hufanya mapito yake kung’aa nyuma yakeHata mtu angedhani kilindi kina mvi.
33. Juu ya nchi hapana aliyefanana naye,Aliyeumbwa pasipo oga.
34. Yeye hutazama kila kitu kilicho juu;Ni mfalme juu ya wote wenye kiburi.