1. Je! Waweza wewe kumvua mamba kwa ndoana?Au, kuufunga ulimi wake kwa kamba?
2. Je! Waweza kutia kamba puani mwake?Au kutoboa taya yake kwa kulabu?
3. Je! Atakusihi sana?Au, atakuambia maneno ya upole?
4. Je! Atafanya agano pamoja nawe,Umtwae kuwa mtumishi wako milele?
5. Je! Utamchezea kama ndege?Au, kumfunga kwa ajili ya wasichana wako?
6. Je! Vikosi vya wavuvi watamfanyia biashara?Watamgawanya kati ya wafanyao biashara?
7. Je! Waweza kuijaza ngozi yake na vyuma vyenye ncha,Au kichwa chake kwa vyusa?
8. Mwekee mkono wako;Vikumbuke vile vita, wala usifanye tena.