Ayu. 40:15-24 Swahili Union Version (SUV)

15. Mwangalie huyo kiboko, niliyemwumba pamoja nawe;Yeye hula nyasi kama vile ng’ombe,

16. Tazama basi, nguvu zake ni katika viuno vyake,Na uwezo wake u katika mishipa ya tumbo lake.

17. Yeye hutikisa mkia wake mfano wa mwerezi;Mishipa ya mapaja yake yanaungamana pamoja.

18. Mifupa yake ni kama mirija ya shaba;Mbavu zake ni kama vipande vya chuma.

19. Yeye ni mkuu wa njia za Mungu;Yeye aliyemfanya alimpa upanga wake.

20. Hakika milima humtolea chakula;Hapo wachezapo wanyama wote wa barani.

21. Hulala chini ya miti yenye vivuli,Mafichoni penye mianzi, na matopeni.

22. Hiyo miti yenye vivuli humfunika kwa vivuli vyao;Mierebi ya vijito humzunguka.

23. Tazama, mto ukifurika, yeye hatetemeki;Hujiona yu salama, ijapokuwa Yordani hufurika hata kinywani pake.

24. Je! Mtu ye yote atamnasa akiwa yu macho,Au, kumtoboa pua yake kwa mtego?

Ayu. 40