Ayu. 40:11-20 Swahili Union Version (SUV)

11. Mwaga mafuriko ya hasira zako,Ukamtazame kila mtu mwenye kiburi, ukamdhili.

12. Mtazame kila mtu mwenye kiburi ukamshushe,Ukawakanyage waovu hapo wasimamapo.

13. Wafiche mavumbini pamoja,Wafunge nyuso zao mahali palipositirika.

14. Ndipo mimi nami nitazikiri habari zako,Ya kuwa mkono wako wa kuume waweza kukuokoa.

15. Mwangalie huyo kiboko, niliyemwumba pamoja nawe;Yeye hula nyasi kama vile ng’ombe,

16. Tazama basi, nguvu zake ni katika viuno vyake,Na uwezo wake u katika mishipa ya tumbo lake.

17. Yeye hutikisa mkia wake mfano wa mwerezi;Mishipa ya mapaja yake yanaungamana pamoja.

18. Mifupa yake ni kama mirija ya shaba;Mbavu zake ni kama vipande vya chuma.

19. Yeye ni mkuu wa njia za Mungu;Yeye aliyemfanya alimpa upanga wake.

20. Hakika milima humtolea chakula;Hapo wachezapo wanyama wote wa barani.

Ayu. 40