Ayu. 40:1-5 Swahili Union Version (SUV)

1. BWANA akafuliza kumjibu Ayubu, na kusema,

2. Je! Mwenye hoja atashindana na Mwenyezi?Mwenye kujadiliana na Mungu, na ajibu yeye.

3. Ndipo Ayubu akamjibu Mungu, na kusema,

4. Tazama, mimi si kitu kabisa, nikujibu nini?Naweka mkono wangu kinywani pangu.

5. Nimenena mara moja, nami sitajibu;Naam, nimenena mara mbili, lakini sitaendelea zaidi.

Ayu. 40