Ayu. 4:1-6 Swahili Union Version (SUV)

1. Ndipo huyo Elifazi, Mtemani, akajibu na kusema,

2. Mtu akijaribu kuzungumza nawe, je! Utaona ni vibaya?Lakini ni nani awezaye kujizuia asinene?

3. Tazama, wewe umewafunza watu wengi,Nawe umeitia nguvu mikono iliyokuwa minyonge.

4. Maneno yako yamemtegemeza huyo aliyekuwa anaanguka,Nawe umeyaimarisha magoti manyonge.

5. Lakini sasa haya yamekufikilia wewe, nawe wafa moyo;Yamekugusa, nawe wafadhaika.

6. Je! Dini yako siyo mataraja yako,Na matumaini yako si huo uelekevu wa njia zako?

Ayu. 4