Ayu. 39:6-18 Swahili Union Version (SUV)

6. Ambaye nimeifanya nyika kuwa nyumba yake,Na nchi ya chumvi kuwa makao yake.

7. Yeye hudharau mshindo wa mji,Wala hasikii kelele zake msimamizi.

8. Upana wa milima ni malisho yake,Hutafuta-tafuta kila kitu kilicho kibichi.

9. Je! Nyati atakubali kukutumikia?Au atakaa katika zizi lako?

10. Je! Waweza kumfunga nyati kwa kamba matutani?Au, yeye atayalima mabonde nyuma yako?

11. Je! Utamtumaini kwa sababu ana nguvu nyingi?Au, utamwachia yeye kazi yako?

12. Je! Utamtumaini kwamba ataileta mbegu yako nyumbani.Na kukusanya nafaka ya kiwanja chako cha kupuria?

13. Bawa la mbuni hufurahi;Lakini mabawa yake na manyoya yake, je! Yana huruma?

14. Kwani yeye huyaacha mayai yake juu ya nchi,Na kuyatia moto mchangani,

15. Na kusahau kwamba yumkini mguu kuyavunja,Au mnyama wa mwitu kuyakanyaga.

16. yeye huyafanyia ukali makinda yake, kana kwamba si yake;Ijapokuwa taabu yake ni ya bure, hana hofu;

17. Kwa sababu Mungu amemnyima akili,Wala hakumpa fahamu.

18. Wakati anapojiinua juu aende,Humdharau farasi na mwenye kumpanda.

Ayu. 39