Ayu. 39:19-22 Swahili Union Version (SUV)

19. Je! Wewe ulimpa farasi uwezo wake?Au, ni wewe uliyemvika shingo yake manyoya yatetemayo?

20. Ndiwe uliyemfanya aruke kama nzige?Fahari ya mlio wake hutisha.

21. Hupara-para bondeni, na kuzifurahia nguvu zake;Hutoka kwenda kukutana na wenye silaha.

22. Yeye hufanyia kicho dhihaka, wala hashangai;Wala hageuki kurudi nyuma mbele ya upanga.

Ayu. 39