8. Hapo wanyama huingia mafichoni,Na kukaa katika mapango yao.
9. Dhoruba hutoka katika vyumba vyake;Na baridi ghalani mwake.
10. Barafu huletwa kwa pumzi za Mungu;Na upana wa maji huganda.
11. Naam, huyatweka mawingu mazito mzigo wa maji;Hulitandika wingu la umeme wake;
12. Nalo hugeuzwa huku na huku kwa uongozi wake,Ili yafanye yote atakayoyaagizaJuu ya uso wa dunia hii ikaayo watu;
13. Kama ni kwa kuonya, au kama ni kwa nchi yake,Au kama ni kwa rehema, ndiye aletaye.
14. Sikiliza neno hili, Ee Ayubu;Simama kimya, uzifikiri kazi za Mungu za ajabu.
15. Je! Wajua wewe jinsi Mungu anavyoziagiza,Na kuumulikisha umeme wa wingu lake?