Ayu. 37:16-24 Swahili Union Version (SUV)

16. Je! Wajua jinsi mawingu yalivyowekwa sawasawa,Hizo kazi za ajabu za huyo mkamilifu wa maarifa?

17. Jinsi nguo zako zilivyo na moto,Hapo nchi ituliapo kwa sababu ya upepo wa kusini?

18. Je! Waweza kuzitandaza mbingu pamoja naye,Ambazo zina nguvu kama kioo cha kuyeyushwa?

19. Utufundishe ni maneno gani tutakayomwambia;Kwa maana hamwezi kuyatengeza kwa sababu ya giza.

20. Je! Aambiwe kwamba nataka kunena?Au mtu angetamani kumezwa?

21. Na sasa watu hawawezi kuutazama mwanga ung’aao mbinguni;Lakini upepo ukipita huzitakasa.

22. Kaskazini hutokea umemetufu wa dhahabu;Mungu huvikwa ukuu utishao.

23. yeye Mwenyezi hamwezi kumwona;Yeye ni mkuu mwenye uweza;Tena mwenye hukumu, na mwingi wa haki, hataonea.

24. Kwa hiyo watu humwogopa;Yeye hawaangalii walio na hekima mioyoni.

Ayu. 37