1. Moyo wangu hunitetema kwayo pia,Nao hutoka mahali pake.
2. Zisikizeni hizo kelele za sauti yake,Na uvumi utokao kinywani mwake.
3. Yeye huituma iende chini ya mbingu zote,Na radi yake hata miisho ya nchi.
4. Baadaye sauti hunguruma;Yeye hunguruma kwa sauti ya ukuu wake;Hazizuii hapo sauti yake isikiwapo.
5. Mungu hunguruma kwa kustaajabisha kwa sauti yake;Hufanya mambo makuu, ambayo hatuwezi kuelewa nayo.
6. Kwani huiambia theluji, Anguka juu ya nchi;Na vivyo manyonyota ya mvua,Na hayo maji ya mvua yake kubwa.
7. Huufunga mkono wa kila binadamu;Ili watu wote aliowaumba wajue.
8. Hapo wanyama huingia mafichoni,Na kukaa katika mapango yao.
9. Dhoruba hutoka katika vyumba vyake;Na baridi ghalani mwake.