Ayu. 36:5-11 Swahili Union Version (SUV)

5. Tazama, Mungu ni hodari, wala hamdharau mtu ye yote;Ana uweza katika nguvu za fahamu.

6. Hauhifadhi uhai wa waovu;Lakini huwapa wateswao haki yao.

7. Yeye hawaondolei macho yake wenye haki;Lakini pamoja na wafalme huwawekaKatika viti vya enzi milele, nao hutukuzwa.

8. Nao wakifungwa kwa pingu,Wakitwaliwa kwa kamba za mateso;

9. Ndipo huwaonyesha matendo yao,Na makosa yao, ya kuwa wametenda kwa kujivuna.

10. Yeye huyafunua masikio yao, wasikie maonyo,Na kuwaagiza warudi kuuacha uovu.

11. Kama wakisikia na kumtumikia,Watapisha siku zao katika kufanikiwa,Na miaka yao katika furaha.

Ayu. 36