19. Je! Mali yako yatatosha, hata usiwe katika taabu,Au uwezo wote wa nguvu zako?
20. Usiutamani usiku,Wakati watu wakatwapo katika mahali pao.
21. Jitunze, usiutazame uovu;Kwani umeuchagua huo zaidi ya taabu.
22. Tazama, Mungu hutenda makuu kwa uweza wake;Ni nani afundishaye kama yeye?
23. Ni nani aliyemwagiza njia yake?Au ni nani awezaye kusema, Wewe umetenda yasiyo haki?
24. Kumbuka kuitukuza kazi yake,Watu waliyoiimbia.
25. Wanadamu wote wameitazama;Watu huiangalia kwa mbali
26. Tazama, Mungu ni mkuu, nasi hatumjui;Hesabu ya miaka yake haitafutiki.
27. Kwani yeye huvuta juu matone ya maji,Yamwagikayo katika mvua kutoka kungeni mwake;
28. Ambayo mawingu yainyeshaNa kudondoza juu ya wanadamu kwa wingi.