15. Yeye humponya aliyetaabika kwa njia ya taabu yake,Na kuyafunua masikio yao kwa maonevu.
16. Naam, yeye angekuongoza utoke katika msibaHata mahali penye nafasi, ambapo hapana msonge;Na kilichowekwa mezani pako kingejaa mafuta.
17. Lakini umejaa hukumu ya waovu;Hukumu na haki hukushika.
18. Basi ujitunze, isije hasira ikakuvuta hata ukafanya mzaha;Wala usikubali ukuu wa ukombozi ukugeuze.
19. Je! Mali yako yatatosha, hata usiwe katika taabu,Au uwezo wote wa nguvu zako?
20. Usiutamani usiku,Wakati watu wakatwapo katika mahali pao.
21. Jitunze, usiutazame uovu;Kwani umeuchagua huo zaidi ya taabu.
22. Tazama, Mungu hutenda makuu kwa uweza wake;Ni nani afundishaye kama yeye?
23. Ni nani aliyemwagiza njia yake?Au ni nani awezaye kusema, Wewe umetenda yasiyo haki?
24. Kumbuka kuitukuza kazi yake,Watu waliyoiimbia.
25. Wanadamu wote wameitazama;Watu huiangalia kwa mbali
26. Tazama, Mungu ni mkuu, nasi hatumjui;Hesabu ya miaka yake haitafutiki.
27. Kwani yeye huvuta juu matone ya maji,Yamwagikayo katika mvua kutoka kungeni mwake;
28. Ambayo mawingu yainyeshaNa kudondoza juu ya wanadamu kwa wingi.