13. Lakini hao wasiomcha Mungu mioyoni hujiwekea hasiraHawalilii msaada hapo awafungapo.
14. Wao hufa wakali vijana,Na uhai wao huangamia katikati ya wachafu.
15. Yeye humponya aliyetaabika kwa njia ya taabu yake,Na kuyafunua masikio yao kwa maonevu.
16. Naam, yeye angekuongoza utoke katika msibaHata mahali penye nafasi, ambapo hapana msonge;Na kilichowekwa mezani pako kingejaa mafuta.
17. Lakini umejaa hukumu ya waovu;Hukumu na haki hukushika.
18. Basi ujitunze, isije hasira ikakuvuta hata ukafanya mzaha;Wala usikubali ukuu wa ukombozi ukugeuze.
19. Je! Mali yako yatatosha, hata usiwe katika taabu,Au uwezo wote wa nguvu zako?
20. Usiutamani usiku,Wakati watu wakatwapo katika mahali pao.