5. Ziangalie mbingu ukaone;Na mawingu yaangalie, yaliyo juu kuliko wewe.
6. Ikiwa umefanya dhambi, umefanya nini juu yake?Yakiwa makosa yako yameongezeka, wamfanyia nini yeye?
7. Ikiwa u mwenye haki, wampa kitu gani?Au yeye hupokea nini mkononi mwako?
8. Uovu wako waweza kumwumiza mtu kama wewe;Na haki yako yaweza kumfaa mwanadamu.
9. Kwa sababu ya wingi wa jeuri wao hulia;Walilia msaada kwa sababu ya mkono wa wakuu.
10. Wala hapana asemaye, Yuko wapi Mungu Muumba wangu,Awapaye nyimbo wakati wa usiku;
11. Atufundishaye zaidi ya hayawani wa nchi,Na kutufanya wenye hekima kuliko ndege za angani?
12. Hulia huko, lakini hapana ajibuye,Kwa sababu ya kiburi cha watu waovu.