Ayu. 35:11-16 Swahili Union Version (SUV)

11. Atufundishaye zaidi ya hayawani wa nchi,Na kutufanya wenye hekima kuliko ndege za angani?

12. Hulia huko, lakini hapana ajibuye,Kwa sababu ya kiburi cha watu waovu.

13. Hakika Mungu hatasikia ubatili,Wala Mwenyezi hatauangalia.

14. Sembuse usemapo wewe ya kuwa humwangalii,Hiyo daawa i mbele yake, nawe wamngojea!

15. Lakini sasa, kwa sababu yeye hakukujilia katika hasira zake,Wala hauangalii sana unyeti;

16. Ndiposa Ayubu hufunua kinywa chake kwa ubatili;Huongeza maneno pasipo maarifa.

Ayu. 35