Ayu. 34:7-13 Swahili Union Version (SUV)

7. Je! Ni mtu gani mfano wa Ayubu,Anywaye mzaha kama maji?

8. Atembeaye na hao watendao uovu,Na kwenda pamoja na watu wabaya.

9. Kwa kuwa amenena, Haimfai mtu lo loteKujifurahisha na Mungu.

10. Kwa hiyo nisikilizeni, enyi wenye fahamu;Mungu asidhaniwe kutenda udhalimu;Wala Mwenyezi kufanya uovu.

11. Kwani atamlipa binadamu kwa kazi yake,Naye atamfanya kila mtu kuona sawasawa na njia zake

12. Naam, hakika, Mungu hatatenda mabaya,Wala Mwenyezi hatapotosha hukumu.

13. Ni nani aliyemwagiza kuiangalia dunia?Au ni nani aliyemwekea ulimwengu huu wote?

Ayu. 34