Ayu. 34:6-10 Swahili Union Version (SUV)

6. Nijapokuwa mwenye haki, nimehesabiwa kuwa mwongo;Jeraha yangu haiponyeki, nijapokuwa sina makosa.

7. Je! Ni mtu gani mfano wa Ayubu,Anywaye mzaha kama maji?

8. Atembeaye na hao watendao uovu,Na kwenda pamoja na watu wabaya.

9. Kwa kuwa amenena, Haimfai mtu lo loteKujifurahisha na Mungu.

10. Kwa hiyo nisikilizeni, enyi wenye fahamu;Mungu asidhaniwe kutenda udhalimu;Wala Mwenyezi kufanya uovu.

Ayu. 34