30. Kwamba huyo mpotovu asitawale,Pasiwe na wa kuwatega watu.
31. Kwani kuna mtu aliyemwambia Mungu,Mimi nimevumilia kurudiwa, ingawa sikukosa;
32. Nisiyoyaona nifundishe wewe;Kama nimefanya uovu sitafanya tena?
33. Je! Malipo yake yatakuwa kama upendavyo wewe, hata ukayakataa?Kwani yakupasa wewe kuchagua, si mimi;Kwa sababu hiyo sema uyajuayo.
34. Watu walio na akili wataniambia,Naam, kila mtu mwenye hekima anisikiaye;
35. Huyo Ayubu amesema pasipo maarifa,Na maneno yake hayana hekima.
36. Laiti Ayubu angejaribiwa hata mwisho,Kwa kuwa amejibu kama watu waovu.