Ayu. 34:20-35 Swahili Union Version (SUV)

20. Hufa ghafula, hata usiku wa manane;Watu hutikisika na kwenda zao,Nao mashujaa huondolewa pasipo mkono wa mtu.

21. Kwani macho yake ya juu ya njia za mtu,Naye huiona miendo yake yote.

22. Hapana weusi, wala hilo giza tupu,Wawezapo kujificha watendao udhalimu.

23. Kwani yeye hana haja ya kumfikiria mtu zaidi,ili aende mbele za Mungu ahukumiwe.

24. Yeye huwavunja-vunja mashujaa pasina kuwachunguza,Na kuwaweka wengine mahali pao.

25. Kwa sababu hiyo yeye huyatafiti matendo yao;Naye huwapindia usiku, wakaangamia.

26. Yeye huwapiga kama watu wabayaWaziwazi mbele ya macho ya wengine;

27. Kwa sababu walikengeuka, wasimwandame yeye,Wasikubali kuzishika njia zake hata moja;

28. Hata wakafanya kilio cha maskini kumfikilia,Naye akasikia kilio cha hao wateswao.

29. Akitoa utulivu yeye, ni nani awezaye kuhukumia makosa?Akificha uso wake, ni nani awezaye kumtazama?Kama hufanyiwa taifa, au mtu mmoja, ni sawasawa;

30. Kwamba huyo mpotovu asitawale,Pasiwe na wa kuwatega watu.

31. Kwani kuna mtu aliyemwambia Mungu,Mimi nimevumilia kurudiwa, ingawa sikukosa;

32. Nisiyoyaona nifundishe wewe;Kama nimefanya uovu sitafanya tena?

33. Je! Malipo yake yatakuwa kama upendavyo wewe, hata ukayakataa?Kwani yakupasa wewe kuchagua, si mimi;Kwa sababu hiyo sema uyajuayo.

34. Watu walio na akili wataniambia,Naam, kila mtu mwenye hekima anisikiaye;

35. Huyo Ayubu amesema pasipo maarifa,Na maneno yake hayana hekima.

Ayu. 34