14. Kama akimwekea mtu moyo wake,Akijikusanyia roho yake na pumzi zake;
15. Wenye mwili wote wataangamia pamoja,Nao wanadamu watarejea tena kuwa mavumbi.
16. Ikiwa una ufahamu, sikia neno hili;Isikilize sauti ya maneno yangu.
17. Je! Atatawala mtu aichukiaye haki hata mmoja?Nawe, je! Utamhukumia mkosa aliye na haki na mwenye nguvu?
18. Je! Inafaa kumwambia mfalme, Wewe u mwovu?Au kuwaambia wakuu, Ninyi ni wabaya?
19. Sembuse huyo asiyependelea nyuso za wakuu,Wala hawajali matajiri kuliko maskini?Kwani wote ni kazi ya mikono yake,
20. Hufa ghafula, hata usiku wa manane;Watu hutikisika na kwenda zao,Nao mashujaa huondolewa pasipo mkono wa mtu.
21. Kwani macho yake ya juu ya njia za mtu,Naye huiona miendo yake yote.