Ayu. 34:1-9 Swahili Union Version (SUV)

1. Tena Elihu akajibu na kusema,

2. Sikilizeni maneno yangu, enyi wenye hekima;Tegeni masikio kwangu, ninyi mlio na maarifa.

3. Kwa kuwa sikio huyajaribu maneno,Kama vile kaakaa lionjavyo chakula.

4. Na tujichagulie yaliyo ya uelekevu;Na tujue wenyewe yaliyo mema.

5. Kwani Ayubu amesema, Mimi ni mwenye haki,Naye Mungu ameniondolea haki yangu;

6. Nijapokuwa mwenye haki, nimehesabiwa kuwa mwongo;Jeraha yangu haiponyeki, nijapokuwa sina makosa.

7. Je! Ni mtu gani mfano wa Ayubu,Anywaye mzaha kama maji?

8. Atembeaye na hao watendao uovu,Na kwenda pamoja na watu wabaya.

9. Kwa kuwa amenena, Haimfai mtu lo loteKujifurahisha na Mungu.

Ayu. 34