1. Tena Elihu akajibu na kusema,
2. Sikilizeni maneno yangu, enyi wenye hekima;Tegeni masikio kwangu, ninyi mlio na maarifa.
3. Kwa kuwa sikio huyajaribu maneno,Kama vile kaakaa lionjavyo chakula.
4. Na tujichagulie yaliyo ya uelekevu;Na tujue wenyewe yaliyo mema.
5. Kwani Ayubu amesema, Mimi ni mwenye haki,Naye Mungu ameniondolea haki yangu;
6. Nijapokuwa mwenye haki, nimehesabiwa kuwa mwongo;Jeraha yangu haiponyeki, nijapokuwa sina makosa.
7. Je! Ni mtu gani mfano wa Ayubu,Anywaye mzaha kama maji?