30. Ili kurudisha roho yake itoke shimoni,Ili atiwe mwanga kwa mwanga wa walio hai.
31. Angalia sana, Ee Ayubu, unisikilize;Nyamaza, mimi nitasema.
32. Kama una neno la kusema, nijibu;Nena, kwani nataka kukuhesabia kuwa na haki.
33. Kama sivyo, unisikilize mimi;Nyamaza, nami nitakufunza hekima.