2. Tazama basi, nimefunua kinywa changu,Ulimi wangu umenena kinywani mwangu.
3. Maneno yangu yatatamka uelekevu wa moyo wangu;Na hayo niyajuayo midomo yangu itayanena kwa unyofu.
4. Roho ya Mungu imeniumba,Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai.
5. Kwamba waweza, nijibu;Yapange maneno yako sawasawa mbele yangu, usimame.
6. Tazama, mimi ni mbele ya Mungu kama ulivyo wewe;Mimi nami nilifinyangwa katika udongo.
7. Tazama, utisho wangu hautakutia hofu wewe,Wala sitakulemea kwa uzito.