Ayu. 33:1-9 Swahili Union Version (SUV)

1. Walakini, Ayubu, nakuomba usikilize matamko yangu,Ukayasikilize maneno yangu yote.

2. Tazama basi, nimefunua kinywa changu,Ulimi wangu umenena kinywani mwangu.

3. Maneno yangu yatatamka uelekevu wa moyo wangu;Na hayo niyajuayo midomo yangu itayanena kwa unyofu.

4. Roho ya Mungu imeniumba,Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai.

5. Kwamba waweza, nijibu;Yapange maneno yako sawasawa mbele yangu, usimame.

6. Tazama, mimi ni mbele ya Mungu kama ulivyo wewe;Mimi nami nilifinyangwa katika udongo.

7. Tazama, utisho wangu hautakutia hofu wewe,Wala sitakulemea kwa uzito.

8. Hakika umenena masikioni mwangu,Nami nimesikia sauti ya maneno yako, ukisema,

9. Mimi ni safi, sina makosa;Sina hatia, wala hapana uovu ndani yangu;

Ayu. 33