1. Walakini, Ayubu, nakuomba usikilize matamko yangu,Ukayasikilize maneno yangu yote.
2. Tazama basi, nimefunua kinywa changu,Ulimi wangu umenena kinywani mwangu.
3. Maneno yangu yatatamka uelekevu wa moyo wangu;Na hayo niyajuayo midomo yangu itayanena kwa unyofu.
4. Roho ya Mungu imeniumba,Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai.
5. Kwamba waweza, nijibu;Yapange maneno yako sawasawa mbele yangu, usimame.