Ayu. 32:4-11 Swahili Union Version (SUV)

4. Basi huyo Elihu alikuwa anangoja ili anene na Ayubu, kwa sababu hao wengine walikuwa wazee kuliko yeye.

5. Hata Elihu alipoona kuwa hapana jawabu katika vinywa vya watu hao watatu, hasira zake ziliwaka.

6. Basi Elihu mwana wa Barakeli, Mbuzi, akajibu, na kusema,Mimi ni kijana, na ninyi ni wazee sana;Kwa hiyo nilijizuia, nisithubutu kuwaonyesha nionavyo.

7. Nilisema, Yafaa siku ziseme,Na wingi wa miaka ufundishe hekima.

8. Lakini imo roho ndani ya mwanadamu,Na pumzi za Mwenyezi huwapa akili.

9. Sio wakuu walio wenye akili,Wala sio wazee watambuao hukumu.

10. Basi nilisema, Nisikilizeni mimi;Mimi nami nitawaonyesha nionavyo.

11. Tazama, niliyangojea maneno yenu,Nilizisikiliza nisikie hoja zenu,Hapo mlipokitafuta mtakalonena.

Ayu. 32