13. Jitunzeni msiseme, Sisi tumepata hekima;Mungu yumkini akamshinda, si mtu;
14. Kwa kuwa yeye hajayaelekeza maneno yake kwangu;Wala sitamjibu mimi kwa maneno yenu.
15. Wameshangaa, hawajibu tena;Hawana neno la kusema.
16. Na mimi, je! Ningoje, kwa sababu hawaneni,Kwa sababu wasimama kimya, wala wasijibu tena;
17. Mimi nami nitajibu sehemu yangu,Mimi nami nitaonyesha nionavyo.
18. Kwa kuwa nimejaa maneno;Roho iliyo ndani yangu hunihimiza.
19. Tazama, tumbo langu ni kama divai iliyozibwa;Kama viriba vipya li karibu na kupasuka.
20. Nitanena, ili nipate kutulia;Nitafunua midomo yangu na kujibu.
21. Tafadhali, nisiupendelee uso wa mtu;Wala sitajipendekeza kwa mtu ye yote.
22. Kwani mimi sijui kujipendekeza;Au Muumba wangu angeniondoa kwa upesi.